“Tunapenda kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Tamasha hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya hali ya juu kwani ulinzi na usalama siku hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man.
Kwa upande wake, Joe Kariuki ambaye ni mratibu mkuu wa tamasha hilo ametumia muda huu kuongea na baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi kuja kunadi bidhaa zao siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao ya kipekee ya kujitangaza bure