Mwanamuziki kinara wa nchini Uganda, Eddy Kenzo amelazwa katika hospitali ya Malcolm nchini humo baada ya kuugua Typhoid na Malaria masaa machache tu baada ya kutoka jiji la Nairobi kwenye show aliyo ifanya huko.
Kwamujibu wa chanzo cha karibu na staa huyo, Eddy Kenzo imemlazimu kusimamisha show zake alizokuwa azifanye mpaka itakapo malizika Pasaka.
Kutokana na kudhoofu sana ndani ya mwili, Dakitari wa mwanamzuiki huyo amemshauri pia apate muda mrefu wa kupumzika kutokana na mwili wake kuchoka zaidi.
Eddy Kenzo anatarajia kutoka hospitali asubuhi hii.