Bondia Many Pacquiao amesema itakua faraja na heshima kwa taifa lake endapo atashiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.
Pacquiao raia wa Ufilipi ameyasema hayo siku moja baada ya shirikisho la kimataifa la masumbwi ya ridhaa AIBA kusema kuwa linarajia kuruhusu ngumi za kulipwa kwenye mashindano za mwaka huu.
Bingwa huyo wa mataji nane katika mashindano ya uzito tofauti tofauti alisisitiza kuwa pambano lake dhidi ya Timothy Bradley mnamo mwezi wa nne mwaka huu lingekua ni la mwisho kwenye masumbwi ya klipwa lakini amesema atarejea endapo AIBA itapitisha pendekezo hilo.
Mfilipino huyo hajafanikiwa kushiriki michuano ya Olimpiki tangu aanze ngumi za kulipwa akiwa na umri wa miaka 19 mnamo mwaka 1995 huku mpinzani wake Floyd Mayweather akiwa ameshiriki miaka 20 iliyopita na kutwaa medali ya shaba huko Atalanta