ZA uso laivu! Staa mwenye mvuto Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi Bongo wataishia kuchambana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram badala ya kutafuta elimu ili siku moja wapate nyadhifa serikalini.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Lulu alisema kwamba, amegundua kuwa elimu ndiyo kila kitu hivyo amewasihi mastaa wenzake waache kuchambana na kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii badala yake watafute njia ya kujikwamua kielimu.
“Jamani mmemuona mwanamama mwenzetu Dk. Tulia alivyojinyakulia unaibu spika? Hiyo ndiyo raha ya elimu. Mastaa kazi kutukanana kwenye mitandao ya kijamii na kuweka picha, mwisho wenu utakuwa hivyohivyo,” alisema Lulu