WEMA SEPETU AMUA KUFUNGA DUKA LAKE LA LIPSTICK

>



Wema Sepetu Amefunguka haya kuhusu Kufunga Duka lake la Kuuza Lipstick za Kiss by Wema Sepetu lililoko Mwenge...

Wemasepetu #KissByWemaSepetu ndio habari ya mjini na nimefarijika kuona jinsi mnavyoniunga mkono...nashukuru sana! 

Sasa kwasababu mawakala ndio njia haraka na nafuu zaidi ya kuwafikishia KISS popote pale mlipo, kuanzia mwezi huu March 2016 tunaweka nguvu zaidi katika kuongeza na kuwahudumia mawakala. 

Kwa mwendo huo basi tunabadilisha mfumo wa biashara namna hii: 

1) TUNAELEKEZA NGUVU ZOTE KWENYE BIASHARA YA KISS. Hii ni bidhaa ya Kitanzania na kwa uzalendo, inabidi tuikazie buti hadi nayo ije kuuzwa nchi za nje kama vile bidhaa za nje zinavyouzika kwetu. 

2) MAUZO YA REJA REJA HAYATAFANYIKA DUKANI KWANGU TENA. Duka litageuzwa kua ofisi ya mambo mengine kuanzia kesho ili kuwapisha mawakala waliotuzunguka, kusiwe na mgongano kibiashara kati yao na sisi. SISI TUTABAKI KUUZA KWA MAWAKALA TU NA WAO WATAWAUZIA NYIE. 

Vitu vingine vyote VINABAKI VILE VILE! 

Bei ya jumla bado elfu 15, bei ya reja reja bado elfu 20, mawakala bado wanahitajika MIKOA YOTE, ile fursa ya kuanza na mtaji mdogo wa elfu 90 ipo pale pale, na wakala mpya ukituma picha zako utarushwa kwenye page yangu kama kawaida. 

Namba za simu bado zile zile: 0789-201-532 na 0759-215-533. 

Tofauti ni kwamba, kuanzia kesho tarehe 2/March/2016, BADALA YA KUJA DUKANI, UTAPIGA SIMU KUWEKA ORDER YAKO YA MZIGO WA JUMLA, ALAFU UTATUMIWA AU KULETEWA kwa gharama nafuu. 

Kwa ufupi: KISS sasa ni ONLINE BUSINESS  

Kama unataka kununua reja reja utumie KISS mwenyewe, uliza tu kwenye comments...#TeamKaziTupoKazini na tutakujibu haraka ujue ukanunue kwa wakala gani

>


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »