Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Shamsa alisema kuwa amenusurika kumpoteza mtoto wake akiwa tumboni kutokana na mitama aliyokuwa akipigwa na mpenzi wake huyo lakini kwa sababu alikuwa anampenda alikuwa habanduki.
“Jamani napinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake wenzangu kwani ilibaki kidogo niharibike ubongo kwa kipigo cha mwanaume huku nikiamini napendwa kumbe ni ujinga mtupu,” alisema Shamsa.