Ishu ya Madawa ya Kulevya, Mrembo Tunda Amkingia Kifua Young D...Asema Haya
MUUZA nyago kwenye video za Bongo Fleva, Tunda Sebastian amejikuta akimkingia kifua mwandani wake, David Genzi ‘Young D’ kutokana na kuhusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya na kudai maneno hayo ni uzushi mtupu.
Akibonga na Showbiz alisema kuwa, anawashangaa watu ambao kila kukicha wamekuwa wakimsakama kipendacho roho wake huyo kuwa ni mtumiaji mzuri wa unga, wakati yeye ndiyo anayemjua vizuri.
“Watu wanapenda sana kuzusha yasiyofaa, sasa kama mimi ndiyo mpenzi wake na sijawahi kumuona kabisa akitumia unga wala kumuhisi hivyo iweje watu wasiomfahamu kiundani wamkomalie hilo suala, hakuna kitu kama hicho, jinsi watu wanavyomfikiria ni tofauti na alivyo,” alisema