rene Uwoya Adai Anapenda Kuigiza ‘Scene’ za Mahaba

>


www.neemayetu.comStaa wa filamu Irene Uwoya amesema anapenda sana kuigiza ‘scene’ za mapenzi katika filamu kwa sababu ni kitu ambacho anaweza kukifanya kwa ukamilifu zaidi.

Muigizaji huyo ambaye alionyesha uwezo mkubwa katika filamu ya Fair Decision, Pretty Girl pamoja na Oprah, amekiambia kipindi cha Uhondo cha EFM kuwa filamu ya Oprah ndio filamu ambayo ilimpa mume.

Kiukweli scene za mapenzi (mahaba) nazipenda kwa kuwa nazifanya vizuri,” alisema Irene. “Kama filamu ya Oprah ndio filamu ambayo ilisababisha nikaolewa, mume wangu alinipigia simu akaniambia nimeona movie yako ya Oprah nataka nikuoe,” alifanunua zaidi.

Lakini ni movie ambayo ilinipa wakati mgumu sana kwa familia yangu, wakiona hii movie si wataniua?. Lakini bahati nzuri baada ya baba kuiona akanipa big up na akanipa ruhusa ya kufanya movie,” aliongeza Irene.

>


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »